Free MP3 Download

522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy

522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy #1
Click image to play video, right click to save image. (Image via youtube.com)
Music Details
Title522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy
MP3 Size3.25 MB (estimated)
Duration03:15
Views1.9K
Sourceyoutu.be/l5D4k8bPn5Q
Description

Mume Anataka Mke Avae Suruwali

Swali:
Ipi hukumu ya kuvaa suruwali mbele ya mume kwa lengo la kumpambia tu na si [kwa lengo] la kujifananisha [na makafiri]?

Shaykh Dr. ´Ubayd bin ´Abdillaah al-Jaabiriy:
Haya ni maneno yako wewe. Makusudio hayahalalishi kilichokatazwa. Kuvaa suruwali mbele ya mume au wengine, huku ni kujifananisha na makafiri. Isitoshe si hata nzuri kwa kuwa inadhihirisha uchi wa mwanamke au nusu ya uchi wake, jambo ambalo ni baya. Na si katika ada ya wanawake wa Kiislamu, si wa mama wa Waislamu wala baada yao kutokana na tunayojua. Na wala sijasoma kama kuna mwanachuoni katoa Fatwa ya kujuzisha hilo. Mwanamke anatakiwa kuvaa vazi la wasaa. Ni kweli mbele ya mume hahitaji kuwa na mtandio, hahitaji Jilbaab. Anaweza kudhihirisha baadhi ya ´Awrah anapokwenda huku na kule. Hili si katika mapambo hata kama baadhi ya watu wajinga watamtaka asifanye hivyo, ima kwa ujinga au kwa Taqliyd kwa baadhi ya watu wamakosa ambao wanafuata kichwa wana-askari wa kikafiri wa mashariki na magharibi. Sisi tunawanasihi mabanati wetu wa kiislamu wajifananishe na Waislamu wa kwanza katika wamama wa Waislamu (wake za Mitume), Maswahabah wa kike, waliokuja baada yao na wa baada yao. Iwe kwenu, kwetu na katika kila kona ya Kiislamu hata walioko nje kuwa na wanawake wazuri wanaoelewa Sunnah na waipende. Hivyo wasije kuwaiga makafiri.

Muulizaji:
Shaykh ikiwa mume atamuomba hili, na kuwa jambo hili analichukulia pambo kwake [mume].

Shaykh Dr. ´Ubayd al-Jaabiriy:
Huyu kageuzwa nyuma na mbele. Huyu kapinda na ni mjinga. Na nadhani ya kwamba kakuzwa kwa musalsalaat (series) na programu za uchi zinazorushwa kwenye Video na nyinginezo. Mimi namnasihi amche Allaah (´Azza wa Jalla) kwa mke wake na amsaidie kwa kumcha Allaah. Wala asimtii. Kwa kuwa hakuna utiifu kwa kiumbe kwa kumuasi Muumba. Kujifananisha na makafiri ni jambo limekatazwa.

Chanzo: [[link stripped - click to show]]

CopyrightAll materials' copyright are belong to their respective owners and/or uploader. This video was uploaded by FatwaZaWanachuoni
LicenseLicensed under YouTube Standard License
Download as MP3
Download as MP4
Alternative
Tags522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy, Download 522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy, Download Video 522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy, Download MP3 522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy, Download 522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy episode terbaru, 522- Mume Anataka Mke Avae Suruwali - Shaykh Dr. ´Ubady al-Jaabiriy terbaru